Serikali imejipanga kukabiliana na kipindupindu Zanzibar

Wizara  ya Afya  Zanzibar imeanza kutoa elimu ya afya katika shehia ambazo  kwa kiasi kikubwa zilikubwa na maradhi ya mripuko ikiwemo kipindupindu  ili  wananchi waanze kuchukua tahadhari  mapema  hasusan katika kipindi hichi cha mvua  za vuli  zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza na Zanzibar24 Mkurugenzi wa kinga na elimu ya afya Zanzibar Dk.Fadhil Muhamed Abdalla amesema Wizara  imejipanga kikamilifu  kukabiliana na  ugonjwa huo kwa utoaji wa  elimu kwa wananchi  ili  kuhakikisha  mvua zinazoendelea  kunyesha  hazisababishi maradhi.

Amesema kuwa miongoni mwa Shehia ambazo zimepewa kipaumbele  katika  utowaji wa elimu  hiyo ni Mtopepo,Daraja bovu,Kinuni na baadhi ya  maeneo ya Vijijini  yaliyozungukwa  na ukanda wa pwani.

Aidha Dk.Fadhil amefahamisha kuwa mbali na utoaji wa elimu  hiyo  pia  Wizara  tayari imeshaweka  vifaa vya kutosha  katika kila kituo  cha  Afya  ili  kukabiliana na  maradhi hayo  endapo  watajitokeza  wagonjwa wa maradhi hayo  ili kuweza kupatiwa huduma za matibabu kwa haraka.

Amina Omar zanzibar24