Jku yadindiwa na kipanga , leo Sailors mzigoni na maafande

Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena jana kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan majira ya Saa 10 za jioni ambapo timu ya JKU waliyovalia jezi nyeusi wakatoka sare ya 0-0 na Kipanga.
Mchezo huo ulikuwa kutokana na ubora wa timu zote mbili huku Mashabiki wengi walijitokeza kuangalia burudani hiyo.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan, mapema saa 8:00 za mchana KMKM watakuwa na kazi kucheza na Mafunzo na saa 10:00 za jioni Black Sailors watacheza na Polisi.
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.