Bausi apiga 4 charawe walipokufa kwa kilimani city

Mshambuliaji Abdillah Seif Bausi amefunga mabao manne na kuiongoza Kilimani City  kuichakaza Charawe kwa mabao 6-1 kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan.
Bausi alifunga mabao hayo katika dakika ya 26, 55, 63 na 65 huku mabao mengine yakifungwa na Ramadhan Junior dakika ya 8 na Abubakar Khamis dakika ya 90.
Bao pekee la Charawe limefungwa na limefungwa na Jeremia Daniel dakika ya 34.
Mara baada ya kumalizika mchezo huo tumefanikiwa kuzungumza na Bausi akielezea furaha yake pamoja na siri kubwa ya kufunga mabao manne pekee ambapo aliondoka na mpira uwanjani hapo.
“Nimefurahi kufunga mabao 4 nashkuru Mungu kwa kuweka rikodi ya kuondoka na mpira leo, lengo langu ni kuisaidia Kilimani City kutoshuka Daraja”. Alisema Bausi.
Nae kocha mpya wa Charawe Ali Bushir ameelezea kipigo hicho kikubwa kwake katika mchezo wake wa kwanza tangu kuifundisha timu hiyo lakini pia ni kipigo cha sita mfululizo tangu kuanza ligi hiyo.
“Ndo mchezo timu yangu bado changa sana naanza kuitengeneza lakini mlinda mlango wetu katuangusha sana, amefungwa mabao mepesi sana, ntaendelea kuitengeneza na kufufua matumaini ya kubakia kwenye ligi kuu”. Alisema Bushir.
Mbali na mchezo huo saa 8 za mchana uwanjani hapo ulipigwa mchezo kati ya Jang’ombe Boys na Zimamoto ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 0-0.
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.