Matukio ya ajali za barabarani yawaliza Wananchi Zanzibar

Jumla ya ajali 4 zimeripotiwa kutokea ndani ya mkoa wa mjini magharibi Unguja kwa mda wa wiki moja ambapo miongoni mwa ajali hizo moja imesababisha kifo.

Akielezea kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi Unguja Ndg. Hassan Nassir Ali amesema ukiacha ajali hizo pia wameyakamata makosa ya barabarani zaidi ya 200, na kati ya hayo makosa 112 yameshapelekwa mahakamani na kutonzwa tozo ya shilingi milioni tatu laki saba na tisiini elfu.