Msichana avuliwa nguo na wazazi wake na kutiwa pilipili sehemu za siri Unguja

Mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 16 mkaazi wa Kizimkazi Dimbani afanyiwa kitendo cha kinyama na wazazi wake wanao mlea wakiwemo mamazake wadogo na bibi yake mzaliwa wa baba kwakumvua nguo zote na kumrandisha mtaani pamoja na kumtia pilipili na chumvi sehemu zake za siri.

Taarifa kutoka kwa Sheha wa shehia hiyo Juma Mkuza Juma amesema kuwa Mtoto huyo alifika nyumbani kwa sheha huyo majira ya saa 12 asubuhi na kumueleza sheha kuwa, alifungwa kamba na wazazi wake hao na badala yake kumpiga na hatimae kumtia pilipili na chumvi katika sehemu zake za siri na baada hapo mtoto huyo baada hapo alikimbilia kwa shangazi yake na alifanikiwa kutiwa asali na maziwa.

Amesema kuwa kisa cha kumfanyia kitendo hicho chakinyama wazazi wa mtoto huyo ni kumtuhumu kuwa amelala kwa mwanamme.

Mtoto huyo amepatiwa matibabu katika hospitali ya Makundushi na kuruhusiwa kwenda nyumbani, na wazazi wake wameshapelekwa katika kituo cha Polisi cha Makunduchi kwa hatua za kisheria.