Sababu ya msichana kutiwa pilipili sehemu za siri na wazazi wake Unguja

Kufuatia tukio la msichana mwenye umri wa miaka 16 Mkaazi wa Kizimkazi kufanyiwa  kitendo cha kinyama na wazazi wake wanao mlea wakiwemo mamazake wadogo na bibi yake mzaliwa wa baba kwakumvua nguo zote na kumrandisha mtaani pamoja na kumtia pilipili na chumvi sehemu zake za siri.

Zanzibar24 imefanikiwa kujua sababu iliyowapelekea wazazi hao ni kwamadai ya kwamba msichana huyo  ameenda kulala kwa mwanaume ndipo walipoamua kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.