Tetemeko la ardhi lauwa watu 200

Tetemeko lenye ukubwa wa 7.3 katika vipimo vya richa limetokea katika eneo la kaskazini mwa Iran na Iraq na kuua watu kadha.

Takriban watu 200 waliuawa katika mkoa ulio magharibi mwa Iran wa Kermanshah, kwa mujibu wa maafisa.

Tetemeko hilo lilizua hofu hadi kusababisha watu kukimbia kutoka majumbani mwao kwenda barabarani.

Misikiti kwenye mji mkuu wa Iraq Baghdad, imekuwa ikifanya maombi kwa kutumia vipasa sauti.

Wengi wa waathiriwa walikuwa ni kwenye mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani.

Kulingana na kituo cha Marekani USGS tetekemo hilo lilitokea umbali wa kilomita 33.9 chini ya ardhi na lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait

Uharibifu umeripotiwa kutokea katika vijiji vinane kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran Morteza Salim.

Baadhi ya vijiji vimekumbwa na matatizo ya nguvu za umeme na mawasiliano yamevurugwa

Makundi ya uokoaji yanatatizwa na maporomoko ya ardhi.

Tetemo hilo lilitokea kilomita 30 kusini magharibi mwa mji wa Halabja karibu na mpaka wa Iran.

Lilitokea umbali wa kilomita 33.9 na lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait.

A map showing an earthquake in the Iran-Iraq border region
Image captionTetemeko nchini Iran na Iraq lawaua zaidi ya watu 200