Mohammed Mmanga anyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi

BEKI kisiki anayekipiga ndani ya klabu ya Polisi, Mohammed Othman Mmanga amechaguliwa kuwa mchezaji bora ndani ya klabu hiyo katika mwezi Oktoba, 2017 kutokana msaada mkubwa alioutoa ndani ya kikosi hicho katika michezo iliyopita ya ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja.
Mmanga ambaye ndio mchezaji pekee kutoka klabu hiyo kuitwa katika timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Hereos), amekuwa na msaada mkubwa katika idara ya ulinzi, na kusababisha timu hiyo kuruhusu mabao 3 katika michezo 6 ya ligi waliocheza.
Mohammed Mmanga (Kulia) akikabidhiwa cheti na kamishna msaidizi muandamizi wa polisi ambae ni Mkuu wa operesheni makao makuu polisi Zanzibar Mihayo M. Msekela
Utaratibu wa kutoa zawadi ya mchezaji bora ndani ya klabu ndio kwanza umeanzishwa kwa mwezi Oktoba na utatolewa kila mwezi, kwa lengo la kuwapa motisha wachezaji ili waweze kujituma zaidi na kuwapa zawadi ya Kikombe pamoja na cheti.
Kwenye msimamo Polisi wapo nafasi ya 7 wakiwa na alama 8 kwa michezo 6 waliocheza ndani ya ligi hiyo yenye jumla ya timu 14.
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.