Waziri aahidi mashine ya kusagia Mwani kwa Wakulima

Waziri wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar Hamad Rashid Mohammed amesema  serikali itazidisha juhudi katika kulisimamia zao la mwani ili liweze kutoa tija  kwa wakulima wazao hilo.

 

Akizungumza na Zanzibar24  kufuatia malalamiko ya wakulima  kuwa na  bei ndogo ya zao hilo   na tatizo la mashine za  kusagia mwani kuwa wa unga ili  kutengeneza bidhaa amesema  kwasasa bei ya mwani inashuka  kutokana na  kuuzwa nje ya nchi lakini  ili kuwarahisishia  wakulima  watawapatia  mashine za kusagia  mwani ambazo  zitasaidia  kuondokana na  tatizo hilo.

 

Amesema kwa  sasa wameshaweka mashine  mbili kwa upande  wa unguja na mbili wanatarajia  kupeleka  pemba  ili kurahisisha  upatikanaji wa unga  wa mwani  ambao   unauzwa  kwa bei ghali.

 

Aidha amewataka wakulima  kuongeza jitihada  juu ya kilimo hicho  kwani serikali inaendeleza kila juhudi  za kuhakikisha  zao hilo  linawanufaisha  wakulima  kutokana na umuhimu wake  katika matumizi mbalimbali ya  binadamu.

Kilimo cha mwani  kimewaajiri wanawake wengi kwa kiasi kikubwa ambapo  watu  Ishirini na tatu elfu  tayari wamejiajiri  kupitia  kilimo hicho kwa unguja na pemba.

Amina Omar Zanzibar24