AT ashinda tuzo mbili nchini Marekani

Msanii wa muziki wa mduara Bongo, AT amefanikiwa kushinda tuzo mbili za B&K Music & Video Music Awards za nchini Marekani ambazo zinahusisha muziki na filamu.

AT ameshinda tuzo hizo kupitia wimbo wake ‘Sili Feel’ ambapo alikuwa akiwania katika vipengele viwili kimoja ni International Artist ambapo alikwa akiwania na wasanii wengine watatu katika mji wa Washington DC.

Na kipengele kingine alichowania ni Best Music Video ambapo alikuwa anawania na wasanii wengine 9.