Habari picha: Meneja wa Hotel ya Misali sun set beach azungumza na Waandishi

NJIA ya waenda kwa miguu wanaotembelea Hoteli ya Misali sun set beach, iliopo Wesha wilaya ya Chakechake Pemba,

 

MENEJA wa Hotel Misali, sun set beach iliopo Wesha Chakechake Pemba, Zahran Juma akizungumza na mwandishi wa Idara ya habari maelezo Unguja, Salum Vuai Issa, aliefika hotelini hapo, kuona maendeleo ya sekta ya Utalii kisiwani humo

 

MTENDAJI wa Hoteli ya Misali sun set beach iliopo Wesha wilaya ya Chakechake, ambae hakupatikana jina lake, akiwasha mashine ya kusukumia maji kwa wananchi wa shehia ya Wesha na hitelini hapo, ambapo kisima cha maji safi na salama kimechimbwa na uongozi wa Hoteli hiyo

 

MTENDAJI wa Hoteli ya Misali sun set beach iliopo Wesha wilaya ya Chakechake, ambae hakupatikana jina lake, akifungua mfereji ambao, upo karibu na kisima cha maji safi na salama, kilichochimba na uongozi wa hoteli hiyo, muda mfupi baada hya kuwasha mashine ya kisima hicho

 

KISIMA kilichochimbwa na uongozi hoteli ya Misali ya sun set beach iliopo Wedha wilaya ya Chakechake, ambacho kwa sasa pamoja na kwamba kinafanya kazi, lakini wananchi wa shehia ya Wesha ambao ndio wanufaika, hakijafanyiwa usafi na kuzungurukwa na majiani

 

MTEMBEZA wageni kwenye hifadhi ya Popo wa Pemba, iliopo kijiji cha Kidike shehia ya Mjini ole, Wilaya ya Chakechake, Omar Aminia Hamad, akionyesha baadhi ya machapisho kwenye ofisi yao, wakati waandishi wa habari walipofika kuitembelea hifadhi hiyo

 

 

MWANDISHI wa habari wa kutoka Idara ya Habari Melezo Unguja, Salum Vuai Issa (mbele) akiwa na dereva wa shirika la Magazeti ya serikali kisiwani Pemba, Ali Suleiman wakipiga picha, kwenye hifadhi ya Popo wa Pemba, iliopo Kidike shehia ya Mjini Ole, wilaya ya Chakechake kisiwani humo

 

MWANDISHI wa habari wa kutoka Idara ya Habari Melezo Unguja, Salum Vuai Issa (nyuma), akiwa na dereva wa shirika la Magazeti ya serikali kisiwani Pemba, Ali Suleiman wakiingia kwenye hifadhi ya Popo wa Pemba, iliopo Kidike shehia ya Mjini Ole, wilaya ya Chakechake kisiwani humo

Picha na Haji Nassor, Pemba.