Idris atoa wimbi la salamu kuhusu Kanumba

Mchekeshaji na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan, ametoa salamu za pole kwa mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa, na kuelezea alivyoyakumbuka maisha mema ya Kanumba wakati akiwa hai duniani na kuongeza kwamba sasa haki yake imepatikana atapumzika kwa amani milele.

Ujumbe huu ndio aliouandika kupitia akaunti yake ya Instagram:
Allah akufanyie wepesi na milele utabaki mioyoni mwetu. Tulifunga njia, kazi na hata kuhema vizuri wengine tulishindwa na tukapata depression kubwa sanaaaa yote kwasababu ulitugusa katika mfano usioelezeka. Naamini haki yako sasa imepatikana na namuombea sana mama yako apewe nguvu na amani ya moyo.