Mamia ya wananchi yafurika mahakamani kuzipinga baa za kusini unguja

Mahakama   ya Vileo Zanzibar imetakiwa    kuwacha  tabia ya  kutoa  vibali vya pombe kiholela    kwani  uwepo  wa baa hizo  bila ya mpango maalum  kunachangia  kuongezeka kwa vitendo  viovu.

Akizungumza  mbele ya Mahakama hiyo Mwanasheria wa kujitegemea Ahmed Mohammed  amesema kasi ya kuongezeka kwa  maovu yakiwemo uhalifu,ukahaba,udhalilishaji  unachangiwa na uwepo wa mabaa nchini  yasiyokuwa na  sifa ya kufanya biashara hiyo.

Amefahamisha  kuwa  licha ya  kuwa serikali inategemea pato lake  kupitia biashara ya pombe lakini  iwatizame wananchi kwa jicho la huruma  kwani wamekuwa waathirika wakubwa wa mabaa hayo  yaliyopo  karibu na makaazi ya jamii.

Amesema   endapo serikali itapunguza  utoaji wa ruhusa za biashara  hiyo  itasaidia  kupunguza utitiri wa mabaa nchini  hasa katika maeneo ya makaadhi ya watu na kulinda maadili  ambayo yanaonekana kupotea kwa kasi kubwa.

Zaidi ya wananchi mia tatu  walijitokeza  kuweka pingamizi zao katika Mahakama ya Vileo  ya Wilaya ya Makunduchi Mkoa wa kusini.

Amina Omar Zanzibar24