Masauni ahamasisha ujenzi wa nyumba za polisi Pemba

Naibu waziri wa mambi ya ndani ya nchi injinia Hamad Yussuf Masauni amekabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 12 za jeshi la polisi kisiwani pemba.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo masauni amesema lengo ni kupunguza changamoto ya makaazi kwa askari polisi kisiwani pemba, ambao wamekuwa na hali ngumu katika makaazi yao licha ya kazi ngumu wanazozifanya za ulinzi wa raia na mali zao.

Amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania imetoa kipaumbele kutatua changamoto za makaazi kwa askari polisi wa kisiwani pemba dodoma na mikoa mipya kwa kutumia wadau ambao wapo tayari kungamkono jitihada hizo

Kwa upande wao wakuu wa mikoa ya kusini na kaskazini pemba mwanajuma majid abdulla na omar khamis othman wamemshukuru naibu waziri huyo wa mambo ya ndani kwa kuchukua juhudi za kutatua changamoto ya makaazi inayokabili askari katika mikoa yao

Zaidi ya familia 50 za askari polisi kisiwani pemba zitanufaika na nyumba hizo zitakapomalizika, kati ya familia 400 wanaohitaji makaazi ambapo mia 200 ni kutoka kusini na mia 200 kaskazini

 

NAFDA HINDI