Wananchi watakiwa kubadili mfumo wa maisha kujiepusha na maradhi ya kisukari

Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar Riziki Pembe Juma amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kula vyakula vinavyoengeza siha katika miili yao na kuepukana na mpangilio mbaya wa vyakula unaoweza kusababisha ongezeko la ugonjwa wa kisukari nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika maadhimisho ya siku ya Ugonjwa wa kisukari, katika ukumbi wa Wizara ya afya Mnazi mmoja mjini Unguja, Kaimu Waziri huyo amesema idadi ya wagonjwa wanougua ugonjwa huo inaengezeka kutokana na wananchi kula vyakula visivyozingatia taratibu za kiafya.

Akizungumzia sababu za kuengezeka kwa ugonjwa huo kwa watu wazima amesema ni pamoja na utumiaji mbaya wa Pombe, Tumbaku na ulaji wa vyakula usiozingatia taratibu za kiafya ikiwemo wananchi kuwa na mwamko mdogo juu ya kutumia mbogamboga na Matunda.

Amesema kutokana na Ugonjwa huo kuleta athari kubwa katika jamii ikiwemo wagonjwa kukatwa baadhi ya viungo vyao, kukumbwa na Ugonjwa wa kiharusi pamoja na kuengezeka kwa vifo vinayotokana na Ugonjwa wa kisukari ni vyema kwa wannchi kuwa tayari kujiepusha na matumizi mabaya ya Vyakula.

Amesema kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Ugonjwa wa kisukari (IDF) limesema Takriban watu Millioni 415 Duniani  wamegundulika kuwa na ugonjwa wa kisukari ambapo kwa mwaka 2040 idadi hiyo inakadiriwa kuengezeka hadi kufikia watu Millioni 642 ambapo nchi zitafanikiwa kuweka mikakati madhubuti ya kujikinga na Ugonjwa huo.

Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar Riziki Pembe Juma ameengeza kuwa  shirika hilo pia limeripoti vifo million 5 vitokanavyo na ugonjwa wa kisukari  kwa mwaka 2015 ambapo idadi imekuwa kubwa ukilinganisha na vifo vitokanavyo na maradhi ya  Ukimwi na kifua kikuu.

Pia ameeleza kuwa katika kila watu kumi na moja kati yao mmoja ana ugonjwa wa kisukari na inakadiriwa ifikapo mwaka 2040 kati ya watu  10 mmoja atakuwa na ugonjwa huo ambapo hali ya maradhi itazidi kuengezeka.

Hata hivyo amesema wanaougua zaidi ugonjwa huo ni Wanaume  na kufikia idadi ya wagonjwa  million 215.2 ambapo wanawake ni million 199.5 .

Amesema  kwa mujibu wa ripoti ta  IDF ya mwaka 2015 imeonesha  kiwango kikubwa wa watoto  kilichofikia  watoto 542,000 waliounduliwa kuugua Ugonjwa huo kwa sababu mbalimbali ikiwemo ulaji usiozingatia mlo kamili.

Kwa Upande wake Mkuu wa kitengo cha Maradhi yasiambukizwa  Omar Mwalimu  amewataka wananchi kuwa kuwa na matumizi mazuri ya dawa za tiba asili zizilizoenea hapa Zanzibar ikiwemo kutumia dawa hizo kwa mpango ili kujiepusha na athari zinazoweza kujitokeza kwa watumiaji hao.

Siku ya Madhimisho ya Ugonjwa wa Kisukari huadhimishwa kila ifikapo Novmber 14 ya kila Mwaka ambapo kwa mwaka huu maadhimisho hayo yana ujembe usemao Chukua tahadhari ili kujikinga na Kisukari.