TAKUKURU yashughulikia suala la Nyalandu

Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru, Brigedia Jenerali, John Mbungo amesema kuwa suala la aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu wamelisikia na wameanza kulifanyia kazi na endapo wakimkuta na hatia watamfikisha kunakostahili.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumanne ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 jana Bungeni aliiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu kwa tuhumu za matumizi mabaya ya madaraka.

Dk Kigwangala alisema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.