Wananchi wametakiwa kujiepusha na ujenzi holela ili kunusuru mali zao

Wananchi wa Wilaya ya kaskazini B wametakiwa kuacha tabia ya ujenzi  holela  katika maeneo ya mabwawa  ili kuepusha athari zinazoweza  kutokea ikiwemo mafuriko wakati wa kipindi  hichi cha mvua zinazonyesha.

Akizungumza na Zanzibar24 Mkuu wa Wilaya hiyo Issa Juma Ali amesema ujenzi holela unachangia  kutokea  kwa maafa ya mafuriko katika maeneo mingi hivyo wanaendelea kutoa elimu  kwa wananchi  juu ya ujenzi bora ambao hautoathiri makaazi ya wananchi wala mali zao.

Amefahamisha kuwa hali  ya mazingira  katika Wilaya yake inaridhisha  kutokana na jitihada  mbalimbali  wanazozichukua za utoaji wa elimu kwa wananchi  juu ya utunzani wa mazingira ikiwemo  kuwa kuchimba mchanga holela na ukataji wa miji ovyo katika vianzio vya maji.

Hivyo amewataka wananchi  kuzidisha jitihada zao  katika kuhifadhi  mazingira  yaliyowazunguka  pamoja  na kufanya  usafi ili kujiepusha na  maradhi   mbalimbali yakiwemo miripuko.

Amina Omar Zanzibar24