Watafiti wa mafuta ya gesi waendelea kufanikisha zoezi lao Unguja

Wataalam wa Jiolojia wanafanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia wanaendelea vizuri na utafiti huo katika Pwani ya Mashariki ya Kisiwa cha Unguja .

Shughuli za utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia zilianza Oktoba 18 mwaka huu baada ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe Balozi Seif Ali Iddi kuzindua rasmi kazi hiyo Oktoba 27, 2017.

Kabla ya utafiti huu wa njia ya mitetemo baharini, mwezi Machi mwaka huu, kulifanyika utafiti wa kukagua miamba ilioko chini ya ardhi ambapo kwa kitaalamu utafiti huo unajulikana “Airborne Full Tensor Gravity Gradiometry Survey” (FTG).

Kampuni ya Bell Geospace Enterprises Limited ya Uingereza ilifanya utafiti huo kwa niaba ya Kampuni ya RAK GAS ya Ras Khaimah, Falme za Kiarabu.

Kwa saa 48 zijazo, Meli tatu za utafiti kutoka Kampuni ya BGP EXPLORER ya China zitakuwa katika eneo la Pwani ya Mashariki mwa Kisiwa cha Unguja.

Mamlaka ya Udhibti wa Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia inasema kwamba kazi inakwenda vizuri sana, ingawa kuna changamoto ndogondogo za shughuli za wavuvi kuwa karibu na maeneo ya utafiti.

Mbali na changamoto ya shughuli za Wavuvi, pia kumekuwa na mawimbi makali.

 

Imetolewa na :-

Dk. Juma Mohammed Salum

 KNY

Mkurugenzi

Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar

Zanzibar

14, Novemba, 2017