Hivi punde: Aliyekuwa Mume wa Uwoya afariki dunia ghafla

Aliyekuwa mume wa msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda, Ndikumana Hamad Katauti (39) amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo.

Chanzo cha kifo cha Ndikumana ambaye kwasasa alikua ni kocha msaidizi wa timu ya Rayon Sports nchini Rwanda bado hakijajulikana.
Ndikumana amewahi kucheza soka Tanzania akiwa na klabu ya Stand United, amewahi kuwa mume wa muigizaji Irene Uwoya na wana mtoto mmoja.
Pole kwa familia na jamaa zake! Inna lillah wa inna ilayh rajiuwn..