Taarifa ya awali kuhusiana na kifo cha aliyekuwa mume wa Irene Uwoya

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa klabu ya Rayon Sports ya nchini Rwanda Gakwaya Olivier ambayo alikuwa akiitumikia Ndikumana kabla ya mauti kumkuta, amesema muda mfupi uliopita kwamba Ndikumana ambaye alikuwa kocha wao msaidizi amefariki kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.
.
“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli,” alisema Olivier na kuongeza kwamba bado wanasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu.