Wengi wao waunga mkono ndoa ya jinsia moja Australia

Waziri mkuu Malcolm Turnbul alisema serikali yake kwa sasa itaruhusu kupitishwa sheria hizo bungeni ifikapo krismasi.

“Watu wa Australia wamezungumza kwa mamilioni na wamepiga kura kwa wingi kura ya ndio kuleta usawa wa ndoa, Bw Turnbull alisema baada ya matokeo kutangazwa.

Zaidi ya watu milioni 12.7 karibu asilimia 79.5 ambao ni wapiga kura walishiriki katika zoezi hilo la majuma 8 ambapo swali moja tu liliulizwa, “sheria ya ndoa inaweza kubadilishwa kuruhusu wapenzi wa jinsia moja kufunga ndo?”

Kura ilionyesha kuwa asilimia 61.6 ya watu walipiga kura kuruhusu wapenzi wa jinsi moja kufunga ndoa.

Wanaounga mkono ndoa za jinsia moja wamekuwa wakisherehekea maeneo ya umma wakiimba na kucheza.