Hii ndio sababu iliyo mfanya mama kanumba kucheka baada ya hukumu ya lulu

Nawashangaa wanaonishangaa mimi kucheka, lakini nawataka wakumbuke kuwa hata mimi nililia mno wakati werngine wakila bata.

Maneno hayo yametamkwa na Flora Mtegoa ambae alikua  Mama wa aliyekuwa mwigizaji mahiri wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba,

Mama Kanumba alisema kuwa, baada ya Lulu kuhukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka miwili kwa kusababisha kifo cha Kanumba bila kukusudia, alijikuta akicheka, lakini hakumaanisha kuwa anafurahia Lulu kwenda jela kwa sababu yeye ni Mkristo hivyo hapaswi kushangilia mabaya ya mwanadamu mwenzake.