Sare dhidi ya libya yamsononesha Erasto Nyoni

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) Erasto Edward Nyoni anaonekana kusononeshwa na sare waliyotoka na Libya baada ya kusema kuwa walitegemea kushinda lakini haikuwa bahati kwao.

Katika mchezo huo wa jana, wa kombe la CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP uliopigwa katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, Kilimanjaro walipata kazi ngumu mbele ya Waarabu wa Libya na kulazimika mchezo huo kutoka sare ya 0-0.

“Tulitegemea kupata ushindi lakini imeshindikana, Libya ni wazuri lakini tunashkuru Mungu kupata alau hiyo point moja”. Alisema Nyoni.

Mchezo wa pili Kilimanjaro Stars itacheza na ndugu zao Zanzibar Heroes siku ya Alhamis ya Disemba 7 saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Kenyatta.

Na: Abubakar Khatib Kisandu.