Tanzania bara yabanwa, Kenya yaanza vyema CECAFA CHALENJ

Wenyeji wa Mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP timu ya Taifa ya Kenya wameenza vyema  baada ya leo kuifunga Rwanda mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa saa 8 za mchana katika uwanja wa Bukhungu huko Kakamega .

Mabao ya Kenya yamefungwa na Maasud Juma na Dancon Otieno.

Na katika uwanja wa Kenyata huko Mjini Machakos timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wakatoka sare ya 0-0 dhidi ya Libya.

Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja kati ya Uganda dhidi ya Burundi Saa 9:00 Alaasiri katika uwanja wa Bukhungu huko Kakamega .

 

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya.