Uchaguzi CCM: Naibu Spika Baraza la Wawakilishi atoa neno kusini Pemba

Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mh. Mgeni Hassan Juma ametoa wito kwa viongozi watakao chaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mkoa huwo kujenga imani ya kukitumikia chama ili kuweza kupata mafanikio makubwa katika chaguzi zijazo.

Mh. Mgeni ameyasema hayo leo huko katika ukumbu wa tibirinzi Chake Chake wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi mkoa huwo unaoshirikisha viongozi na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa kusini pemba.

Amesema lengo la chama chochote cha siasa ni kupata ushindi, hivyo amewataka viongozi hao wapya  watakao chaguliwa wawe dira katika kukipatia ushindi chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Aidha amewataka viongozi na wana CCM kuendelea kuinadi ilani ya chama cha mapinduzi kama nihatua moja wapo yakuunga mkono juhudi za viongozi wote wa chama hicho.

Nafasi zitakazo gombaniwa katika uchaguzi huwo wa Mkoa wa Kusini Pemba ni pamoja na nafasi ya mwenyekiti ccm mkoa, wajumbe wanne wa halmashauri kuu ya taifa, katibu mwenezi mkoa na wajumbe wa halmashauri kuu mkoa.