Wolper afunguka mapenzi yake kwa Alikiba

Msanii wa Filamu Bongo, Jacqueline Wolper  amelazimika kuzungumzia ukaribu na Alikiba baada ya kuandika ujumbe wenye kusisimua katika kumtakia kheri ya siku ya kuzaliwa kwa Alikiba.

Ujumbe alioandika Wolper kwa Alikiba ulisomeka, “Happy birthday to you Ally!I love you and you know that!More life Kiperete wangu…!”.

“Hatuna urafiki lakini ni mtu ambaye namjua toka zamani kabla ya yeye hajawa staa na mimi sijawa staa, kwa hiyo tunajuana zamani lakini pia hatujawahi kukoseana adabu, kutukanani kwenye mitandao au kukosoana” Wolper ameiambia FNL ya EATV.

“Kuna vitu ambavyo ameniheshimu, unapomu-wish mtu kuna feeling, kile kitu ambacho kinakujia moyoni inabidi ukifanye na kimeshakujia, so ilinijia na kuna vitu nilikumbuka nikasema ngoja niandike kwa sababu ni kweli kutokana na tulivyokuwa tunaishi miaka ya 2000 huko” amesisitiza.

Kipindi cha nyuma wawili hawa walishakuwa katika uhusiano wa kimapenzi.