Mamilioni ya pesa yaliteketezwa kwa Mazishi ya Mandela Afrika Kusini

Mazishi ya aliyekuwa rais wa zamani Afrika kusini ,Nelson Mandela yanadaiwa kukumbwa na ufisadi mkubwa ambao unadaiwa kutekelezwa na viongozi wakuu nchini humo.

Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo imebaini kuwa takriban dollar millioni 22 ilitumika vibaya wakati wa matayarisho ya mazishi ya Mandela miaka minne iliyopita.

Ripoti hiyo inasema kwamba viongozi hao walivuja pesa na kukiuka taratibu zilizowekwa huku ikisemekana kwamba gharama za bidhaa ziliongezwa maradufu na matumizi ya mazishi kutajwa kuwa ya juu sana kwa mfano shati za kumbukumbu ya mazishi zilinunuliwa kwa dollar 25 badala ya dollar 19 .

Hata hivyo ripoti hiyo imetaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahalifu waliofanya jambo hilo la kushangaza katika jamii.