Kodi yazua utata Baraza la manispaa na Wafanyabiashara Unguja

Wafanyabiashara wa Samaki katika soko la darajani wamelilalamikia  baraza la Manispaa  kwa kuwatonza kodi  mara mbili  hali inayosababisha  usumbufu  na kuwarudisha nyuma kimaendeleo.

Wakizungumza na Zanzibar24  wamesema  baraza hilo limekuwa likiwatonza kodi  kila siku  asubuhi na jioni  jambo linalowapa  ugumu katika  kujikwamua na umaskini.

Hivyo wameliomba baraza hilo kuangalia utaratibu wake  inaotumia katika ukusanyaji wa kodi ili  na wao  waweze kukidhi mahitaji  yao na kupambana na umaskini.

Nae Mkuu wa Mapato wa baraza la Manispaa Salma Abdillah Omar amesema  hakuna mfanyabiashara anayetozwa  kodi mara mbili katika sehemu zao za kufanyiabiashara.

Amesema kutokana na idadi kubwa ya wafanyabiashara katika soko hilo baraza limeamua  kugawa  zamu za kukusanya kodi  kwa wafanyabiashara  wa asubuhi  na join ili waendeshe  shughuli zao bila usumufu.

Amina Omar Zanzibar24