Mh. Mnyika arudisha imani kwa Chadema

Mbunge wa Kibamba  John Mnyika amefanikiwa kurejesha imani na furaha  kwa baadhi ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuonesha kuguswa na kile kinachoendelea kwa Wabunge, Madiwani na wafuasi 34 wa Chama hicho kutaka wapewe dhamana kwani ni haki yao kimsingi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter wafuasi wa Mnyika ambao wanaaminika pia kuwa wafuasi wa chadema wamempongeza Mnyika kwa kuonesha uimara wake kwa kusimama na wabunge wa Chadema katika kipindi cha matatizo.

Kwenye mtandao wake Mnyika amendika “Nasimama na wabunge wetu wawili; Ndugu Peter Lijuakali na Susan Kiwanga, Madiwani wetu wawili na wanachama wetu 34 ambao kwa mara ya pili sasa bado wanakataliwa kupewa dhamana tangu Novemba 26. Dhamana ni haki ya msingi! Tusirudie makosa na uhuni”.

Hata hivyo baada ya ujumbe huo Mnyika alipokea maoni tofauti yakisema
Nebo Yolam : At last am in peace of mind again, thanks maana ukimya wako ulinipa was mkubwa

Mzalendo Halisi‏: Nimetamani kuweka likes millioni kwenye hii twitt, @jjmnyika hujajua tu umenipa amani kiasi gani,,

Fanuel Simon‏: Tunaimani na wewe usituangushe vijana wenzako(ni vijana wangapi leo kwenye hii nchi wanakutazama kama role model wao) waangalie na wao.