Mtulia amekimbilia CCM kwasababu ya njaa zake

Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Kinondoni George Mwingila amepinga vikali sababu zilizotolewa na aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia na kusema hazina ukweli wowote bali akubali kuwa njaa zake ndizo zilizomkimbiza CCM.

Akizungumza leo na Wanahabari Mwingila amesema kwamba Mtulia kuhama CUF ambayo ipo chini ya mwamvuli wa UKAWA kwa madai anakubali kazi rais anayofanya, ni uongo mtupu kwani angeweza kumuunga mkono rais akiwa ndani ya chama chake na siyo kuhama.

“Kwenye ilani yetu ya uchaguzi tuliyoinadi 2015 hapakuwa na ajenda ya kubomolea watu nyumba zao na wala hatukuwa na ajenda ya kununua wanachama wa upinzani wala viongozi wake. Sasa uakuja unasema kwamba unamuunga rais na Chama chake mkono  kwa nini usiseme wazi tu kwamba ni njaa zako. Kama kweli unamuunga Rais mkono kwa nini usimuunge bila kuhama.Mwingila

Ameongeza kwamba “Mbona hata ndani ya Chadema wapo wanaomuunga rais mkono kwa baadhi ya mambo na hata ndani ya CCM wapo wanaotuunga CHADEMA pamoja na Mh. Lowassa mkono mbona wao hawaahami?  Ukweli ni kwamba umefanya usaliti kwa sababu ya njaa.

Mbali na hayo Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kinondoni amesema alichokifanya Mtulia ni Usaliti wa hali ya juu na asubiri mshahara wa dhambi hiyo hapa hapa duniani kabla hajaonja mauti.