Picha: Mama Walezi wa vijiji vya Watoto yatima kutunukiwa Dhahabu

Rais wa  vituo vya kulelea watoto yatima  duniani  Siddartha Kaul  anatarajiwa kuwatunuku zawadi maalumu Mama  walezi wanaowalea watoto katika  vijiji vya kulelea watoto SOS   ikiwemo Zanzibar, Arusha na Dar es salamu.

Zawadi hiyo anayotarajiwa  kuwatunuku   wa mama hao katika hafla yake ya  ziara  aliyoifanya  katika kijiji cha watoto SOS  Mombasa Mjini unguja  ni Pete za dhahabu ikiwa ni hisani   ya malezi kwa watoto hao.

Katika hafla hiyo anatarajiwa  kuwa mgeni rasmi Mama Mwema Shein  na baadhi ya viongozi mbali mbali  katika ngazi ya chama na Serikali.

Amina Omar Zanzibar24