SMZ imetenga kiasi hiki, kwa ajili ya utanuzi na kuimarisha huduma za hospital ya Chakechake

 Jumla ya shilingi Millioni mia tatu na hamsini zimetengwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya utanuzi wa Hospitali ya Chakechake ili kuimarisha  huduma za Afya hospitalini hapo.

Akijibu swali la Nyongeza katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani Nnje kidogo ya mji wa Zanzibar ,Waziri wa Afya Zanzibar Mahmod Thabit Kombo amesema kujengwa kwa Hospitali hiyo kutawasaidia wagonjwa kuondokana na Usumbufu wanaoupata ikiwemo ukosefu wa sehemu za kupumzikia.

Kukamilika kwa hospital hiyo pia kutawawezesha wahudumu  wa hospitalini hapo kufanya kazi kwa ufanisi na katika maeneo yenye nafasi wakati wanapowahudumia wagonjwa.

Amesema amema ujenzi huo utaanza rasmin baada ya kukamilika kwa Ramani na masuala ya kiufundi ambapo majengo mawili yaliopo hospitalini hapo yatabomolewa na kujengwa mapya ya ghorofa ili wagonjwa waweze kunufaika na miundombinu ya kisasa.

Akizungumzia suala la ufinyu wa Tanuri la Kuchomea taka hospitalini hapo Waziri Kombo amesema Wizara yake italipatia Ufumbuzi tatizo ili kupunguza kero la kuenea kwa Moshi katika makaazi ya watu jambo ambalo linawapa wasisi wasi mkubwa wananchi juu ya Afya zao.

Aidha ametowa wito kwa wananchi kuwa wastahamilivua wakati wizara ikiendelea na jitihada hizo na kuwataka kuondowa wasiwasi kwa moshi unaotokana katika tanuri hilo kutokna na moshi huo hauna sumu na hauleti madhara ya afya kwa wanannchi.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.