Wema Sepetu baada ya kurudi CCM: Najihisi nimekatishwa tamaa

Baada ya msanii wa filamu, Bongo Wema Sepetu kurudi CCM kutokea Chadema, hatimaye amezungumzia hilo.

Wema amesema hawezi sana kulizungumzia hilo kwa sababu maamuzi yalishafikiwa lakini anajihisi kukatishwa tamaa.

“Yaani it so complicated najikuta sipo kwenye position ya kuielezea in simple English or Swahili, siwezi lakini tubaki tu tunaomba Mwenyenzi Mungu kwamba everything it will be ok one day inshallah” Wema ameiambia K Fm, Rwanda.

“I am strong, nisingekuwa strong nisingekuwa hapa sasa hivi najaribu kusali kwa hii hali, muda mwingine kama binadamu inakuwa inanivunja moyo najihisi nimekatishwa tama, yaani ok!  acha nimuachie Mungu” ameongeza.

February 24 mwaka huu Wema alijiunga na Chadema akitokea CCM na December Mosi alitangaza kurudi CCM.