Bunge laidhinisha ndoa za jinsia moja

Ndoa za jinsia moja sasa zitakuwa halali  baada ya bunge kusitisha mswada wa kihistoria kwenye bunge la waakilishi nchini Australia.

Wabunge wengi walipiga kura kubadilisha sheria ya ndoa siku nane baada ya kura kama hiyo katika bunge la Senate.

Kura hiyo ilizua shangwe bungeni na kusababisha furaha na hata nyimbo.

Matokeo hayo yanafikisha kikomo mjadala mkali kwa karibu muongo mmoja kuhusu swala hilo.

Watu wengi wanaounga mkono ndoa za jinsia moja walisafiri kwenda Canberra kushuhudia matokeo ya buge la chini.

Serikali ya waziri mkuu wa Australia Malcolm Turnbull ilileta mswada huo baada ya watu kuupiga kura kwa wingi kuunga mkono ndoa za jinsia moja kwenye kura ya kitaifa.

Zaidi ya watu milioni 12.7 karibu asilimia 79.5 ya wapiga kura wakishiriki kwenye kura ya maoni ya kitaifa iliyodumu kipimdi cha wiki sita.