Haji Manara: Wakipata uanachama watakwenda World Cup

Mdau mkubwa wa soka na msemaji wa klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam Haji Manara ameweka wazi hisia zake juu ya Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes baada ya kuitandika bila huruma timu ya Taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars mabao 2 kwa 1 mapema leo huko katika Uwanja wa Kenyatta nchini Kenya.

Manara amefunguka kuwa hana shaka kuwa kama Zanzibar itapata uanchama wa CAF na FIFA basi watakwenda AFCON na World Cup kabla ya Tanzania Bara.

Haji Manara ameyasema hayo kupitia ukurasa wake binafsi katika mtandao wa Instagram kama inavosomeka hapo chini:

Sina shaka hata chembe.Zbar wakipata uanachama wa kudumu CAF na FIFA.watakwenda World Cup na Afcon kabla ya Tanzania Bara….najua wengine mtaudhika.ila hyo ni fact..wao 2 cc 1 ..hongera @zanzibarfootballassociation🙏🙏

Mapema leo Timu ya Zanzibar Heroes wameifunga Timu ya Tanzania Bara magoli mawili kwa moja huku wakionesha soka safi lililowaduwaza timu ya Tanzania Bara.