Hatimaye shilole afunga ndoa : Nuh Mziwanda amtupia dongo

Hatimaye msanii wa Bongo Fleva, Shilole amefungua ndoa na mpenzi wake Ashraf Uchebe huko Masaki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.
Staa huyo alikuwa akisisitiza kufunga ndoa mwaka huu lakini watu walikuwa wakichukulia poa kwa sababu si mara ya kwanza kutoa kauli kama hiyo lakini jana Desemba 6 akafanya kweli.
Baada ya picha za harusi kusambaa mtandaoni aliyekuwa mpenzi wa Shilole hapo awali, Nuh Mziwanda ameandika ujumbe katika ukurasa wa Instagram ambao unaweza kutafsiriwa kama ametupa kijembe kwenye ndoa hiyo.  Nuh ameandika;
Alie LaLa na BiBi harusi’wiki Moja KabLa ya harusi’Na wala sio Bwana Harusi’Bado mnanishauri harusi 😏 (all girls are pretenders )
Alichokiandika Nuh Mziwanda ni mistari kutoka kwenye wimbo wa Mwana FA ‘Bado Nipo Nipo’ ambao ulitoka takribani miaka 10 iliyopita.