Mama Mwanamwema Shein: Walezi zidisheni mapenzi pindi munapotoa huduma kwa watoto yatima 

Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mama Mwanamwema Shein amewataka walezi wanaowalea watoto katika vituo mbalimbali nchini kuzidisha mapenzi  wanapotoa huduma za malezi kwa watoto yatima ili kuwapa faraja watoto hao.

Akizungumza katika halfa ya kuwavisha pete za dhahabu baadhi ya wakina  Mama waliofanya kazi hiyo kwa ufanisi katika  Vijiji vya kulelea watoto yatima SOS amesema malezi bora kwa watoto  ni muhimu kwani yatawajenga na kuwa raia wema.

Pete hizo za dhahabu zilitolewa na Rais wa SOS  duniani Siddhartha Kaul  ikiwa ni zawadi kwa mama hao waliojitolea kuwalea watoto yatima ambao kwa mujibu wa sheria za kitaifa na kimataifa wanahitaji huduma bora ili wasijihisi wapweke.

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Vijiji vya SOS  Anatoli Rugaimukam  amesema jukumu la kuwalea watoto  hasa wenye mahitaji maalumu si  la mama peke yao bali ni la jamii nzima,nakuitaka jamii isijisaau katika kutoa ushirikiano katika malezi ya watoto hasa yatima.

 Mapema  Rais wa SOS Siddhartha Kaul amesema lengo la kuwatunukia pete mama hao  ni shkrani za malezi bora walioyatoa kwa watoto hao takribani ya miaka 20  katika vijiji vya SOS Zanzibar,Arusha na Dar es salamu.

Jumla ya mama walezi 18 wametunukiwa pete za dhahabu ikiwa ni shukrani zao za malezi bora za huduma bora  walioyatoa kwa watoto wa SOS  zaidi ya miaka 20 katika vituo.

 Amina Omar Zanzibar24