Mtoto aliyeibwa apatikana baada ya miaka 40

Mwanamke ambaye alichukuliwa kutoka kwa mama yake baada ya kuzaliwa nchini Argentina, ameunganishwa na familia yake na kundi linalofahamika kama Grandmothers of the Plaza de Mayo.

Adriana, mwenye miaka 40, ambaye aliomba jina lake la pili kutofichuliwa alitambuliwa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa DNA.

DNA yake ililingana na ya familia ya wazazi wake ambao walitoweka wakati wa utawala wa kijeshi nchini Argentina.

Adriana ndiye mtoto wa 126 kupatwa na Grandmothers, ambao wanaendesha kampeni kwa niaba ya waathiriria wa “Dirty War”.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari, Adriana alisema kuwa wakati watu waliokuwa wamemlea walikufa, aliambiwa na mtu mwingine kuwa yeye hakuwa mtoto wao wa kuzaliwa.

Adriana (C), a girl who was forced into adoption during the Argentinian dictatorship (1976-1983), Buenos Aires, Argentina, 05 December 2017.Adriana (wa katikati)

Alifanyiwa uchunguzi wa DNA na baada ya miezi minne hakupata DNA iliyolingana na yake, kutoka kwa ile inayohifadhiwa na Grandmothers ya watu walitoweka au kuuliwa na utawala wa kijeshi.

“Nilianza kufikiri kuwa nilitelekezwa, nilikanwa au kuuzwa kwa sababu hawakuwa wananitaka.” alisema Adriana.

Lakini siku ya Jumatatu alipata simu kutoka tume ya kitaifa ya haki ya kutambuliwa, ikimuambia kuwa walikuwa na ujumbe wangependa kumpa yeye.

Adriana alienda mara moja na kuambiwa kuwa alikuwa binti wa Violeta Ortolani na Edgardo Garnier, wote walitoweka wakati wa utawala wa kijeshi.

A woman named Adriana (she wished not to release her current last name), who was taken away from her mother during the 1976-1983 Argentine dictatorship, speaks during a news conference at the human rights organization Abuelas de Plaza de Mayo (Grandmothers of Plaza de Mayo) headquarters in Buenos Aires, Argentina December 5, 2017Wanaharakati walishika picha za wazazi wa Adriana waliotoweka mwaka 1977.