MV Mapinduzi II yasababishia serikali hasara ya milioni hamsini

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewataka wananchi Wanaotumia usafiri wa Majini wa Meli ya Mv Mapinduzi II kutokuwa na wasisi wakati wa safari kutokana na meli hiyo kuwa na tatizo la kukatika umeme mara kwa mara.

Akijibu swali katika katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Chukwani Nnje ,Naibu Waziri wa Ujenzi,mawasiliano ,na Usafirishaji muhammed Ahmad amesema matatizo yanyojitokeza katika meli hiyo ni hitilafu za kawaida ambazo hazikatishi safari.

Akizungumzia sababu ya kukatisha Safari meli hiyo amesema kunatoka na ukosefu wa vipuri vya dharura katika meli hiyo na kusababisha meli hiyo kusitisha huduma za usafiri.

Amesema katika kukabiliana na tatizo hilo shirika la Meli kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi tayari imeshaagiza vipuri kwa awamu vitakavyo saidia kuondoa tatizo hilo.

Aidha amesema mafundi tayari wapo wanaendelea na jitihada za kukabiliana na hitilafu mbali mbali zinazojitokeza katika meli hiyo ili kuimarisha huduma ya Usafiri kwa abiria.

Tangu kununuliwa meli hiyo ni mara ya pili kuharibika na Kuisababisha hasara Serikali ya Zaidi ya shilling Milioni hamsini zinazotumika kwa matengenezo jambo ambalo linasababisha ukosefu wa usafiri wa uhakikia kwa wananchi.