Chozi ndege Mwenye rangi na sauti ya kusisimua

Chozi ni familia ya ndege wadogo ambao wenye rangi kali na zenye kung’aa juani mithili ya metali.

Manyoya ya kati ya mkiani ni marefu sana katika baadhi ya aina yao, wana mdomo mrefu uliopinda amabo huutumia kwa kutoa wadudu katika matundu yao.

chozi

Kwa kawaida Chozi ni ndege wanaoishi maisha ya mume mmoja mke mmoja ambapo hukaa pamoja kwenye kiota kimoja na vifaranga, kwa kawaida jike ndiye anayewajibika kujenga kiota ambako hutaga yai moja hadi mawili na baadhi ya aina hufika mayai manne ambayo huyaatamia (kulalia)  kwa siku kadhaa.

Madume hufanya kazi mbili kubwa moja ikiwa ni kumsaidia jike kuwalisha vifaranga baada ya kuanguliwa pili kubwa na muhimu zaidi ni kulinda eneo la malisho.

Chozi ndege wazuri wanaovutia wanapotembea bustani yenye maua mazuri na kuipamba kwa rangi zao nzuri.

Na: Yoda – 1990