SMZ yataja sehemu inayo tarajia kujenga eneo lakudumu kwa ajili ya maonesho ya kibiashara

Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Wameiomba Wizara ya Biashara ,Viwanda na Masoko kuendelea kutowa elimu  kwa vijana wanaofanya kazi katika Viwanda vidogo vidogo ili bidhaa zao ziweze kuendana na mahitaji katika soko la ajira.

Wakichangia mswada wa Sheria ya kuanzisha wakala wa maendeleo ya viwanda Vidogo vidogo na Vya kati katika kikao cha Baraza la wawakilishi ,Wajumbe hao wamesema vijana kumekuwa na mwamako wa kujishughulisha na bidhaa ndogondogo lakini wanakabiliwa na tatizo la kukusa Elimu.

Wamesema pindipo Elimu itatolewa na Vijana na wananchi wanaoofanya bidhaa zao katika Viwandanda vidogovidogo watasaidia kuimarisha ubora wa bidhaa wanazozalisha ili ziweze kutumika duniani kote.

Akijibu hoja za Wajumbe hao Waziri wa Wizara hiyo Balozi Amina Salum Ali amesema serikali inaendelea na azma yake ya kutoa elimu kwa wafanya biashara mbali mbali ili waweze kuzalisha bidhaa nzuri zinazoendana na mahitaji.

Akizungumzia suala la kuimarisha Biashara na ujasiriamali Nchi Balozi Amina amesema tayari serikali imekusudia kujenga maeneo ya Maonesho ya kudumu yatakayotumiwa na Wafanya biashara hao katika kuuza na kutangaza Bidhaa zao.

Amesema eneo hilo litakalojengwa katika kijiji cha Nyamanzi litakuwa na Ofisi ,Maeneo ya Maonesho na Nyumba za kulala wageni zitakazowapa fursa Wafanya Biashara wa Zanzibar na Nnje ya Zanzibar kushiriki Maonesho.

Na;Fat-hiya Shehe Zanzibar24.