Ukosefu wa vifaaa kwa wakulima wa miche ya karafuu ni tatizo

Umoja wa Wakulima wa Miche ya Mikarafuu Donge Vijibweni Uwamido wameiyomba  Serikali  kuwasaidia  vifaa vitakavyowasaidia  katika kuikuza miche wanayoipanda.

Akizungumza na Zanzibar24 Katibu wa Uwamido Ameir Abasi Ameir amesema wamejikusanya pamoja katika kupanda  mikarafuu lakini wanakabiliwa na ukosefu wa vifaa  vinavyotumika katika uatikaji wa miche hiyo ikiwemo mabero,glove,ndoo na keni za kumwagilia maji.

Amesema kukosekana kwa vifaa hivyo  kunarejesha nyuma  jitihada zao ikizingatia  kuwa kuua kwa miche hiyo kunahitajika huduma za uhakika.

Kwaupande wake  Mkuu wa Kitengo cha mazao ya Biashara na Matunda kutoka Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Badru Kombo Mwavura ameutaka umoja huo kufuata taratibu za kisheria za usajili ili kupata  misaada kutoka  taasisi zinazoshughulikia uimarisha wa zao hilo.

Amina Omar Zanzibar24