utowaji wa dhamana  kiholela  inachangia unachangia kuongezeka kwa kesi za udhalilishaji kwa wanawake na watoto 

Jeshi laPolisi Zanzibar limetakiwa  kupunguza utoaji wa dhamana kwa  watuhumiwa wa  vitendo vya udhalilishaji  ili kupunguza  mrudikano wa kesi hizo kuchukua mda mrefu katika kutolewa hukumu.

Akizungumza katika Maadhimisho ya siku kumi na sita ya kupiga  vita vitendo vya udhalilishaji  yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Zanzibar Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Shadia Mohamed Suleiman amesema  endapo Jeshi la polisi litafanya kazi  kwa uwadilifu  bila ya muhali itawaza kufanikisha lengo la serikali kupiga vita udhalilishaji nchini.

Amesema  uwepo wa dhamana  kiholela  inachangia  kuwapa  kipaumbele wadhalilishaji  kuendelea kudhalilisha wanawake na watoto kila kukicha  hali ambayo  inaathiri  jamii kisaikologia.

Kwaupande wake Afisa wa dawati la kijinsia la Makao Makuu ya Polisi Rahma Ali Salum akisoma risala iliyoandaliwa na Madawati  ya jinsia amesema  katika kukabiliana na vita ya udhalilishaji nchini lazima serikali iwe tayari  kuunda tume ya uchunguzi kama ilivyounda tume nyengine ili kushughulikia kesi zote katika kupatiwa ufumbuzi na kutambua chanzo cha tatizo.

Nae Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Hassan Nassir ametoa wito kwa jamii  kuzidisha mashirikiano ya kuziripoti kesi za udhalilishaji katika madawati  ya jinsi ili  watendaji na washughulikiaji  wa kesi hizo kuweza kuzitolea hukumu kwa mujibu wa sheria za nchi.

Jumla ya kesi Mia nne na nne zimeripotiwa katika madawati mbalimbali ya mkoa wa mjini magharibi Januari hadi Septemba mwaka huu.

Jeshi laPolisi Zanzibar limetakiwa  kupunguza utoaji wa dhamana kwa  watuhumiwa wa  vitendo vya udhalilishaji  ili kupunguza  mrudikano wa kesi hizo kuchukua mda mrefu katika kutolewa hukumu.

Akizungumza katika Maadhimisho ya siku kumi na sita ya kupiga  vita vitendo vya udhalilishaji  yaliyoandaliwa na Jeshi la Polisi Zanzibar Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Shadia Mohamed Suleiman amesema  endapo Jeshi la polisi litafanya kazi  kwa uwadilifu  bila ya muhali itawaza kufanikisha lengo la serikali kupiga vita udhalilishaji nchini.

Amesema  uwepo wa dhamana  kiholela  inachangia  kuwapa  kipaumbe  wadhalilishaji  kuendelea kudhalilisha wanawake na watoto kila kukicha  hali ambayo  inaathiri  jamii kisaikologia.

Kwaupande wake Afisa wa dawati la kijinsi la Makao Makuu ya Polisi Rahma Ali Salum akisoma risala iliyoandaliwa na Madawati  ya jinsia amesema  katika kukabiliana na vita ya udhalilishaji nchini lazima serikali iwe tayari  kuunda tume ya uchunguzi kama ilivyounda tume nyengine ili kushughulikia kesi zote katika kupatiwa ufumbuzi na kutambua chanzo cha tatizo.

Nae Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Hassan Nassir ametoa wito kwa jamii  kuzidisha mashirikiano ya kuziripoti kesi za udhalilishaji katika madawati  ya jinsi ili  watendaji na washughulikiaji  wa kesi hizo kuweza kuzitolea hukumu kwa mujibu wa sheria za nchi.

Jumla ya kesi Mia nne na nne zimeripotiwa katika madawati mbalimbali ya mkoa wa mjini magharibi Januari hadi Septemba mwaka huu.

Amina Omar Zanzibar24