Mwanafunzi wa kike akataliwa kushiriki mahafali kisa kuvaa hijabu

Mwanafunzi wa sheria nchini Nigeria amazuiwa kuingia kwenye sherehe za mahafali yao kutokana na yeye kusisitiza kuvaa hijab kama kujisitiri wakati wa sherehe hizo.

Amasa Firdaus, ambaye alifuzu kutoka chuo cha Ilorin, alizuiwa kuingia ukumbini kusherehekea mahafali kwenye mji mkuu wa Nigeria Abuja ambapo sherehe zilikuwa zikifanyika.

Alikataa kuvua hijab yake akisitiza kuwa angevaa kofia juu ya hijab yake na kusemwa kuvaa hivyo ni kuenda kinyume na vazi ramsi lililowekwa na vyuo vya sheria.

Tukio hilo limeibua hisia kubwa katika mitandao ya kijamii.

Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alisema kuwa Bi Firdaus ana haki ya kufanya hivyo.