Yanga yaanza vyema Mapinduzi CUP

Klabu ya Yanga imeanza vyema kombe la Mapinduzi baada ya kupata ushindi wa magoli 2 kwa 1 dhidi ya Mlandege, mchezo uliofanyika majira ya Saa 2:30 usiku katika Uwanja wa Amani.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Juma Mahadhi mnamo dakika ya 6 na 36 huku goli pekee la Mlandege likipachikwa na Omari Makame mnamo dakika ya 47.