Zimamoto yatepeta mbele ya Singida United Mapinduzi CUP

Timu ya Singida United, leo hii imefanikiwa kuianza vizuri michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyoanza kutimua vumbi Desemba 29 mwaka jana mjini Unguja baada ya kuitandika Zimamoto FC.
Mchezo ulizokutanisha timu hizo umefanyika katika Uwanja wa Amaan ambapo Singida United imeibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Mabao ya Singida United ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza michuano huyo yamefungwa na Deus Kaseke katika dakika ya saba, Dany Usengimana dakika ya 21 pamoja na Kigi Makasi dakika ya 81.

 

Kwa upande wa Zimamoto  mabao yake yote mawili yamefungwa na Ibrahim Hamad Ahmada Hilika katika daika ya 39 na 84.