Mbunge wa Chakechake Pemba aainisha mafanikio ya Ahadi zake

Mbunge wa jimbo la chakechake kisiwani Pemba kwa tiketi  ya chama cha wananchi  CUF  Mh Yussuf Kaiza  Makame amesema kuwa kitendo  bora katika uwongozi ni kuahidi katika maendeleo na kisha kuzitekeleza ahadi kwa wananchi kama ulivyoahidi.

Kauli hiyo aliitoa leo katika ofisi mpya ya mbunge huyo huko chakechake mjini wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali juu ya kutazama vipi kiongozi bora anatakiwa awe kwa wananchi wake pamoja na utekelezaji wa ahadi alizoziahidi kupitia nafasi ya ubunge aliyopewa na wananchi wa jimbo la chakechake.

Kaiza alisema , wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi wa 2015 wakati akiomba ridhaa za wananchi kumchagua , aliahidi mambo mbali katika sekta tofauti hivyo kama kiongozi bora kwa wananchi wake aliamua kwa makusudi kutelekeza yale aliyoyaahidi.

Alisema katika miaka miwili ya uwongozi wake kwa kiasi ameanza  kufanikiwa kutelekeza ahadi zake alizoziahidi kama vile kuweka mazingira sawa katika sekta ya elimu, maji, barabara, michezo, kuwawezesha vijana na akina mama,  kujenga miundombinu imara kama vile madaraja ya kuvukia na kubwa zaidi la kufungua afisi ya mbunge jiomboni.

Akizichambua moja baada ya moja ahadi alizoanza kuzitekeleza, akianzia na elimu alisema ,alifanikiwa kuchangia fedha taslim na vifaa kwa skuli ya msingi chanjaani,  hii ni  baada ya kuwaona wanauhitaji wa kusaidiwa na lengo kuu ni kuwafanya watoto wasome katika mazingira mazuri.

“nyote mutakua mashahidi ,kuna siku bank ya NMB walitoa fedha na vifaa vya maabara kuwaaidiwa wanafunzi na skuli yao ya shamiani , ile ilikua ni kupitia mimi ” alisema Kaiza.

Pamoja na hayo alisema , hivi sasa jumla ya shilingi milioni 15 zimeshatengwa kwaajili ya ujenzi wa mabanda matatu ya skuli ya msingi Pondeani.

Akizungumzia upande wa huduma ya umeme alisema, kuna vijiji vitano ndani ya jimbo la chakechake siku zote vilikua vinakosa umeme lakini kupitia uwongozi wa mbunge huyo hivi sasa wanaanza kufurahia huduma hiyo “vijiji vyenyewe ni pamoja na mtoni kupandisha michakaini, mtoni bandani, matuleni vijiji viwili na kijiji kimoja ni cha polepole njia ya shungi kuelekea tundauwa” alisema mbunge huyo.

Mbunge huyo wa chakechake pamoja na mambo mengineyo alisema, kwa kiwango kikubwa pia alifanakiwa kutatua baadhi ya changamoto za wananchi wa jimbo lake katika sekta mawasiliano ya barabara  alau kwa kuanzia na kifusi katika baadhi ya maeneo pamoja na kujenga madaraja na vivuko vidogo vidgo.

“tumejenga daraja maeneo ya mtoni bandani,wanafunzi wanapita kutokea mtoni kwenda michakaeni,walikua wanapata usumbufu kabla ya uwepo wa daraja hilo” alisema kaiza.

Akijibu suala kutoka kwa waandishi wa habari juu ya kiasi cha pesa kilichotumika katika matumizi ya utelekezaji wa baadhi ya ahadi zake alizema “zaidi ya  shilingi milioni sitini zimetumika kufanikisha utekelezaji huo” alisema Kaiza

Katika hatua nyengine mbunge wa chakechake alisema, jambo kubwa aliloliahidi kwa wananchi wake ni kufungua ofisi yake jimboni na sasa ameshafanikisha hilo maeneo ya mjini chakechake hivyo aliwataka wananchi kufika katika ofisi hizo pale kutakapotokea shida ya kutaka kuoananae kwani afsi hiyo ni kwaa jili ya wananchi wa jimbo la chakechake.

Sambamba na hayo amewataka viongozi ,kujenga moyo wa kuwatumikia kidhati wananchi wao pamoja na kutekeleza ahadi walizoziahidi kwani ndiko kutakapoonyesha matumaini ya wananchi baada ya kukuchagua.

Mwisho kabisa alitoa wito kwa wapiga kura wake wawe wastahamilivu,  bado anaendelea kupigia mbio changamoto zilizobakia na ahadi alizoziahidi ili kuzitekeleza kiukamilifu  kwani kubaadhi ya maeneo bado kuna matatizo na anayajua .