Mzanzibar aunda helkopta
Mzanzibari Said Omar maarufu Sugu Mkaazi wa tomondo Wilaya Magharib B amefanikiwa kuunda Helkopta ambayo ameionesha leo katika viwanja vya maisara Mjini Unguja huku akisubiri kibali kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini TCAA.
Akizungumza na Zanzibar24 amesema amechukua hatua ya kuunda helkopta akiwa na lengo la kuuonesha umma uwezo wake wa ubunifu wa vifaa vya moto ambapo hapa nchini hamna utaalamu huo.
Akizungumzia kuhusu utengenezaji wa helkopta hiyo amesema imemugharimu zaidi ya Shillingi Milioni saba hadi kukamilika kwake na imechukua miaka minne tokea 2015 hadi 2018 katika utengenezwaji wake.
Amesema helkopta hiyo inavifaa vyote muhimu vinavyohitajika kuwemo ndani ya helkopta ikiwemo mashine za kisasa, life jaketi, vifaa muhimu ambavyo vinavyohitajika wakati wa safari.
Ubunifu huo wa Mr sugu si mara ya kwanza kubuni vifaa vya moto bali hii ni awamu ya tatu ambapo awali miaka ya nyuma alibuni Baluni ya kuruka hewani iliyochukua abiria, Gari ambapo alizawadiwa na serikali Shilingi Milioni Mbili na hivi sasa amebuni helkopta hiyo ambayo iliyomugharimu zaid ya Milioni 7.
Picha zaidi za helkopta hiyo