74 Watunukiwa Nishani na Rais wa Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi  Dk. Ali Mohammed Shein amewatunuku  nishani   watumishi wa serikalini na wanasiasa  wa  chama cha mapinduzi  kutokana na utendaji wao bora  katika harakati  mbalimbali katika serikali yake.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa nchi ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi  Issa Haji Ussi Gavu amesema Jumla ya Watendaji 74 ambao  kati yao 43 wamewatunukia  nishani  ya Mapinduzi  kwa kufanya   vyema  katika chama   na 31 wametunukiwa  nishani ya utumishi  uliotukuka katika  serikali.

Akiwataja miongoni mwa  watu hao waliotunukiwa nishani ya mapinduzi ni Marehemu Amina Saadi Ferouz ambae ni mwanasiasa  mkongwe, Ramadhani Abdalla Ali ambae ni muumini wa mapinduzi, Haji  Machano  Haji ambae pia ni mwanasiasa mwanzilishi  wa umoja wa vijana  na Wengine waliotunukiwa nishani ya Utumishi Uliotukuka ni Marehemu  Sheikh Harith Bin Khelef  Mufti wa Zanzibar na ofisa muandamizi wa serikali, Marehemu Othman Bakar Othman aliyekuwa Mwenyekiti wa tume  ya utumishi serikalini na ofisa muandamizi  wa serikali Yussuf  Khamis Yussuf Mkuu wa Wilaya na Ofisa mwandamizi wa serikali  na Ahmada Khamis Hilika Ofisa  muandamizi  wa serikali.

Watendaji hao waliotunukiwa nishani na rais wa Zanzibar wanatarajiwa kuvishwa nishani hizo  tarehe 11 katika viwanja vya ikulu mjini Zanzibar na Rais Dr Shein.