Ushoga wa Shamsa Na Aunt Ezekiel wazua mjadala

Ushosti uliochipuka na kukolea hivi karibuni wa mastaa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford na Aunt Ezekiel, umeibua mambo huku wengi wakihoji ulikoanzia kwa sababu haukuwahi kuwepo na kwamba hawaendani.

Mastaa hao walisema kuwa, wanashangazwa na watu wanaohoji urafiki wao huo ulianza lini na wengine wakisema hawapendezani ambapo Shamsa alisema kuwa, wanaoongea hivyo wamekosa vitu vya kufanya.

Kwa upande wa Aunt amesema kuwa wanaojadili urafiki wake na Shamsa hawana jipya kwani alishakuwa na marafiki wangapi hadi waujadili huo wa sasa? “Nimeshakuwa na marafiki wengi sana. Kwa nini wajadili urafiki wangu na Shamsa?” Alihoji Aunt.